Music is a supporting component of many kinds of entertainment and most kinds of performance. |
Muziki ni kiungo kinachoauni aina tofauti za burudani na michezo mingi ya kuigiza. |
For example, it is used to enhance storytelling, it is indispensable in dance and opera, and is usually incorporated into dramatic film or theatre productions. |
Kwa mfano, muziki hutumika wakati wa kupeana hadithi, kwenye densi na pia hujumuishwa kwenye filamu na michezo ya kuigiza. |
Music is also a universal and popular type of entertainment on its own, constituting an entire performance such as when concerts are given. |
Muziki pia ni njia maarufu sana ya burudani duniani kote, haswa katika maonesho na tafrija. |
Depending on the rhythm, instrument, performance and style, music is divided into many genres, such as classical, jazz, folk, rock, pop music or traditional. |
Muziki hugawanywa kwenye aina tofauti kulingana na mtindo, ala zinazotumika na utendaji, kama vile classical, jazz, folk, rock, pop na muziki wa kitamaduni. |
Since the 20th century, performed music, once available only to those who could pay for the performers, has been available cheaply to individuals by the entertainment industry which broadcasts it or pre-records it for sale. |
Tangu karne ya ishirini muziki wa tafrija, uliosikilizwa tu na walioweza kulipa wasanii, umeweza kupatikana kwa bei nafuu kutoka kwenye viwanda vya burudani ambavyo hutangaza na hurekodi na kuuza. |
The wide variety of musical performances, whether or not they are artificially amplified, all provide entertainment irrespective of whether the performance is from soloists, choral or orchestral groups, or ensemble. |
Tafrija nyingi za muziki, zilizo na ala ua zisizo nazo, hutoa burudani iwapo ni maonesho kutoka kwa mwanamuziki mmoja, wawili au vikundi vya wanamuziki. |
Live performances use specialized venues, which might be small or large; indoors or outdoors; free or expensive. |
Tafrija za muziki hufanyiwa mahali maalumu ambapo panaweza kuwa padogo au pakubwa; ndani au nje; bure au kwa malipo. |
The audiences have different expectations of the performers as well as of their own role in the performance. |
Watazamaji huwa na matarajio tofauti kwa wanamuziki na pia mahali pao kwenye tafrija. |
For example, some audiences expect to listen silently and are entertained by the excellence of the music, its rendition or its interpretation. |
Kwa mfano, hadhira zingine husikiliza kimya huku wakiburudishwa na uzuri wa muziki, mtindo wake au tafsiri yake. |
Other audiences of live performances are entertained by the ambience and the chance to participate. |
Hadhira nyingi za tafrija huburudishwa na mandhari na kuwa na fursa ya kuhudhuria. |
Even more listeners are entertained by pre-recorded music and listen privately. |
Wasikilizaji wengi zaidi huburudishwa kwa muziki uliorekodiwa na husikiliza kibinafsi. |