The Lord of the Flies contains many examples of symbolism which Golding has incorporated to show a deeper level to the main, mostly straightforward, storyline that reveals his thoughts on the nature of humanity and evil. |
Katika kitabu "The Lord of the Flies" Golding ametumia ufananisho sana kueleza kwa undani maoni yake kuhusu utu wa binadamu na uovu ambayo ni jambo kuu analofafanua katika kitabu chake. |
Below are some of the main symbols used in the book, but there are plenty more for you to discover yourself. |
Yafuatayo ni baadhi ya mifano yanayojitokeza aliyotumia, hata hivyo ukisoma kitabu hicho kwa makini utapata mifano mengi zaidi. |
Among such symbols may be included such small or natural seeming events like the coral reef, (Submarine warfare, surrounding of Britain by German U-boats?) or the "great fire", which may represent the first world war, ("We shall never commit to this savagery again"). |
Baadhi ya mifano aliyotumia ni ya ni vitu vidogo vidogo au vitu vya asili kama miamba ya matumbawe (huenda alivitumia kuashiria vita vya manowari, yaani jinsi Wajerumani walitumia manowari yaliyoitwa U-boat kuwazunguka na kuwafungia Waingereza.) au "moto mkubwa" ambao huenda unarejelea vita vya kwanza vya ulimwengu, (Hatutawahi kamwe kuruhusu unyama wa aina hii utendeke tena") |
Blood is another symbol Golding uses extensively, although what he uses it for is open to interpretation. |
Golding anafananisha damu na vitu vingi, hata hivyo, hasemi moja kwa moja damu inaashiria nini katika visa vyote, kwa hivyo msomaji anaweza kujiamulia mwenyewe. |
The different styles of leadership shown by Jack and Ralph symbolize democracy and dictatorship, much like as depicted in George Orwell's Animal Farm where he used pigs to symbolize the USSR's communist leaders. |
Aina mbali mbali za uongozi zinazoelezwa na Jack na Ralph yanaashiria uongozi wa kidemokrasia na wa kiimla, jinsi tu inavyoonyeshwa katika kitabu cha Animal Farm iliyoandikwa na George Orwell ambapo viongozi wa ukomunisti, wa Muungano wa Sovieti au USSR walifananishwa na nguruwe. |
The imaginary beast that frightens all the boys stands for the primal instinct of savagery that exists within all human beings. |
Yule mnyama wa kuwaziwa anayewaogopesha vijana wote anaashiria silka ya unyama iliyo ndani ya kila mwanadamu. |
The boys are afraid of the beast, but only Simon reaches the realization that they fear the beast because it exists within each of them. |
Vijana wote wanamwogopa mnyama huyo, hata hivyo ni Simon peke yake anayegundua kwamba wanamwogopa yule mnyama kwa sababu wao wote wana unyama ndani yao. |
As the boys grow more savage, their belief in the beast grows stronger. |
Jinsi vijana hao wanavyoendelea kuwa wakatili, ndivyo wanavyoendelea kumwamini zaidi yule mnyama. |
By the end of the novel, the boys are leaving it sacrifices and treating it as a totemic god. |
Kitabu inapoelekea kuisha inapata kama vijana wanamtolea yule mnyama dhabihu tena wanaitendea kama mungu wao. |
The boys’ behavior is what brings the beast into existence, so the more savagely the boys act, the more real the beast seems to become. |
Tabia ya vijana hao ndiyo inayowafanya waamini kuwepo kwa huyo mnyama, jinsi wanavyozidi kuwa wakatili, ndivyo mnyama huyo anavyoendelea kuwa halisi zaidi kwao. |
The boys "become" the beast when they kill Simon. |
Ni kana kwamba vijana hao "wanageuka" na kuwa yule mnyama wanapomuua Simon. |
Golding describes the savages' behavior as animal like; the savages dropped their spears (man's tool) and "screamed, struck, bit, tore. There were no words, and no movements but the tearing of teeth and claws." |
Golding anaeleza kwamba vijana hao walitenda kama wanyama; wakatili hao walitupa chini mikuki yao (kifaa cha mwanadamu) "walipaaza sauti, walimpiga Simon, walimuuma na kumrarua rarua. Neno halikutamkwa, walikaa tuli, sauti pekee iliyosikika ni ya meno na makucha yakimrarua Simon!" |