| Technology plays an increasingly significant role in improving access to education for people living in impoverished areas and developing countries. |
Teknolojia ina wajibu muhimu zaidi wa kuboresha ufikiaji wa elimu kwa watu walio katika maeneo yaliyo na miundo-msingi duni na nchi zinazoendelea. |
| Charities like One Laptop per Child are dedicated to providing infrastructures through which the disadvantaged may access educational materials. |
Mashirika ya misaada kama One Laptop per Child yamejitolea kutoa miundo-msingi ambayo wasio na uwezo mkubwa kimaisha wanaweza kufikia nyenzo za elimu. |
| The OLPC foundation, a group out of MIT Media Lab and supported by several major corporations, has a stated mission to develop a $100 laptop for delivering educational software. |
Wakfu wa OLPC, ambao ni kikundi cha MIT Media Lab kwa msaada wa mashirika makuu kadhaa, limeanzisha misheni ya kuunda kompyuta ndogo kwa dola 100 za kuwasilisha programu za elimu. |
| The laptops were widely available as of 2008. |
Kompyuta ndogo hizi zilianza kupatikana zaidi mwaka wa 2008. |
| They are sold at cost or given away based on donations. |
Zinauzwa kwa gharama fulani au zinapeanwa kulingana na michango. |
| In Africa, the New Partnership for Africa's Development (NEPAD) has launched an "e-school program" to provide all 600,000 primary and high schools with computer equipment, learning materials and internet access within 10 years. |
Katika Afrika, shirika la New Partnership for Africa's Development (NEPAD) limezindua "mpango wa elimu ya mtandaoni" ili kutoa ufikiaji intaneti, nyenzo za elimu na vifaa vya kompyuta kwa shule zote 600,000 za msingi na sekondari katika kipindi cha miaka 10. |
| An International Development Agency project called nabuur.com, started with the support of former American President Bill Clinton, uses the Internet to allow co-operation by individuals on issues of social development. |
Shirika la Maendeleo ya Kimatifa linalojulikana kama nabuur.com, lililoanzishwa kwa msaada wa aliyekuwa Rais wa Marekani Bill Clinton, hutumia intaneti ili kuwaruhusu watu mahususi washiriki katika masuala ya maendeleo ya jamii. |
| India is developing technologies that will bypass land-based telephone and Internet infrastructure to deliver distance learning directly to its students. |
India inunda teknolojia zitakazokua bora zaidi kuliko miundo-msingi ya ardhini ya simu na intaneti ili kutoa elimu ya mbali moja kwa moja kwa wanafunzi wake. |
| In 2004, the Indian Space Research Organisation launched EDUSAT, a communications satellite providing access to educational materials that can reach more of the country's population at a greatly reduced cost. |
Mwaka wa 2004, Shirika la Utafiti wa Angani la India lilizindua EDUSAT, ambayo ni setilaiti ya mawasiliano inayotoa ufikiaji wa nyenzo za elimu ambazo zinaweza kufikia idadi kubwa ya watu nchini kwa gharama iliyopunguzwa zaidi. |