| Technology plays an increasingly significant role in improving access to education for people living in impoverished areas and developing countries. |
Teknolojia inaendelea kushikilia nafasi muhimu katika kufanikisha upatikanaji wa elimu miongoni mwa watu wanaoishi katika maeneo maskini na mataifa yanayoendelea. |
| Charities like One Laptop per Child are dedicated to providing infrastructures through which the disadvantaged may access educational materials. |
Mashirika ya misaada kama vile One Laptop per Child yamejitolea kuhakikisha kuwepo kwa miundombinu ambayo kwayo waliokumbwa na changamoto wanaweza kupata vifaa vya kielimu. |
| The OLPC foundation, a group out of MIT Media Lab and supported by several major corporations, has a stated mission to develop a $100 laptop for delivering educational software. |
Wakfu wa OLPC, kikundi kinachotokana na MIT Media Lab na kuungwa mkono na mashirika makubwa kadhaa, lina lengo lililowekwa wazi la kuunda kipatakilishi kinachogharimu $100 cha kutolea programu za kielimu. |
| The laptops were widely available as of 2008. |
Vipakatalishi hivi vilipatikana sana kuanzia 2008. |
| They are sold at cost or given away based on donations. |
Vinauzwa kwa bei fulani au kutolewa kama michango. |
| In Africa, the New Partnership for Africa's Development (NEPAD) has launched an "e-school program" to provide all 600,000 primary and high schools with computer equipment, learning materials and internet access within 10 years. |
Barani Afrika, shirika la New Partnership for Africa's Development (NEPAD) limeanzisha mradi wa masomo ya mtandaoni inayotoa vifaa vya tarakilishi na vifaa vya kusoma kwa shule zote 600,000 za msingi na za upili na pia kuziwezesha shule hizi kupata mtandao katika kipindi cha miaka kumi. |
| An International Development Agency project called nabuur.com, started with the support of former American President Bill Clinton, uses the Internet to allow co-operation by individuals on issues of social development. |
Shirika moja la Maendeleo la Kimataifa liitwalo naabur.com, ambalo lilianzishwa kwa msaada wa Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton, hutumia mtandao ili kuendeleza ushirikiano wa watu binafsi kuzungumzia masuala ya maendeleo ya jamii. |
| India is developing technologies that will bypass land-based telephone and Internet infrastructure to deliver distance learning directly to its students. |
India inakuza teknolojia ambazo hazitahitaji matumizi ya simu za nyaya wala miundombinu ya mtandao ili kutoa mafunzo ya mbali moja kwa moja kwa wanafunzi wake. |
| In 2004, the Indian Space Research Organisation launched EDUSAT, a communications satellite providing access to educational materials that can reach more of the country's population at a greatly reduced cost. |
Katika mwaka wa 2004, Shirika la Utafiti wa Anga la India lilizindua EDUSAT, setelaiti ya mawasiliano inayofanikisha kuwepo kwa vifaa vya kielimu vinavyoweza kufikia sehemu kubwa ya wananchi wake kwa bei nafuu sana. |